Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pasipo amani wakulima hawana imani kuwekeza katika kilimo:FAO

Pasipo amani wakulima hawana imani kuwekeza katika kilimo:FAO

Shirika la kilimo duniani FAO limefikia wakulima takriban milioni 3 nchini Sudan Kusini mwaka 2014 waliokumbwa na changamoto ya mzozo wa wenyewe kwa wenyewe.

FAO katika juhudi zake ilitoa mbegu, nyavu za uvuvi, vifaa vya mifugo na majiko yanayojali mazingira kwa ajili ya wanawake wanaosafiri maeneo hatari wakitafuta kuni. Licha ya kwamba hatua zimepigwa, masoko bado yanayumba yumba na njia za usafirishaji zimefungwa wakati mzozo ukiendelea.

Mkuu wa FAO nchini Sudan Kusini ,Sue Lautze amesema kwamba upatikanaji wa amani ndio hatua ya kwanza ya kutatua ukosefu wa usalama wa chakula.

“Tunahitaji amani ili masoko haya yarudi ili chakula kiweze kuwasilishwa kutoka vituo vya biashara na tunahitaji amani ili watu wakae nyumbani na waendeleze kilimo. Upanzi wa mimea ni uwekezaji wa juu na nahisi kwamba iwapo itamlazimu mtiu kukimbia, watu hawatawekeza katika kilimo, na iwapo hawatalima kutaakua na visa Zaidi vya utapiamlo na maradhi yanayotokana na utapiamlo na njaa aidha umasikini utaenea kwa wasudan kusini"