Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yasambaza vifaa kwa ajili ya Msimu wa Baridi kwa wakimbizi Afghanistan

UNHCR yasambaza vifaa kwa ajili ya Msimu wa Baridi kwa wakimbizi Afghanistan

Kama sehemu ya msaada wa kuhimili msimu wa baridi kali kwa familia 32,000 waliofurushwa makwao nchini Afhganstan , Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR), kwa kushirikiana na wizara inayohusika na wakimbizi na watu waliorejea makwao, MoRR, na wadau wengine wameaanza kusambaza vifaa vya kukabiliana na baridi kwa wakazi wa Kabul wanaoishi katika mazingira magumu.

Katika vituo viwili vya usambazaji vilivyoko Bagh-e-Zanana na Pul-i-Charkhi, vilivyoko mjini Kabul, UNHCR na MORR walisambaza mavazi ya joto, hasa kwa watoto na vifaa vya jikoni kwa familia 2,300 ya wakimbizi na watu waliorejea makwao hivi karibuni.

Katika Mkoa wa Kati, ikiwa ni pamoja Kabul, Panjsheer, Ghazni, Wardak, Logar, Kapisa na mikoa Parwan, UNHCR imesambaza vifaa vya kukabiliana na msimu wa baridi kali kwa familia 6,000, ambapo familia 4500 walifurushwa makwao hivi karibuni sawa na familia 1500 wanaoishi katika mazingira magumu.Walengwa wa usaidizi huo ni wakimbizi na watu waliorejea makwao hivi karibuni wanaoishi mjini Kabul wakati wa msimu wa baridi sawa na walemavu na wazee.