Hakuna Visa vya Ebola Iraq: WHO

Hakuna Visa vya Ebola Iraq: WHO

Uchunguzi wa Shirika la Afya Duniani, WHO imedhibitisha kuwa hakuna kisa cha Ebola nchini Iraq. Hii ni kufuatia uvumi katika vyombo vya habari nchini Iraq kwamba kisa cha Ebola kimepatikana Mosul, Mkoani Ninewa.

Uchunguzi huo ulifanywa kupitia mitandao iluiyopo ya ufuatiliaji na mawasiliano kupitia mamlaka ya afya na vyanzo vya matibabu katika hospitali ya Ibn Sina ilioko Mosul.

Eneo la Mosul limekuwa chini ya himaya ya kundi linalotaka kuweka dola la Kiislamu cha ISIL tangu mwezi Juni 2014.

Katika siku za hivi karibuni, Ebola imesababisha vifo vya zaidi ya watu 8000 Afrika. Wizara ya Afya ya Iraq na WHO wameongoza juhudi zao za ufuatiliaji ili kuhakikisha ugunduzi wa mapema na usimamizi salama wa watu wanaoshukiwa kuambukizwa Ebola nchini.