Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bila juhudi za pamoja haiwezekani kuitokomeza Fistula: CCBRT

Bila juhudi za pamoja haiwezekani kuitokomeza Fistula: CCBRT

Harakati za kuwanusuru wanawake wenye ugonjw wa Fistula unaosababishwa na ukosefu wa huduma stahiki wakati wa kujifungua zinahitaji jitihada za pamoja. Ni kauli ya meneja mawasiliano wa shirika lisilo  la kiserkali linalojihusisha na afya CCBRT Abdul Kajumulo.

Kauli ya mkuu huyo wa mawasiliano inakuja wakati ambapo Umoja wa Mataifa kupitia baraza kuu hivi karibuni umetoa wito wa kukomeshwa kwa ugonjwa huo ambao umeathiri wanawake takribani milioni 2 kote duniani.

Katika mahojiano na Joseph Msami wa idhaa hii Kajumulo anasema kampeni dhidi ya Fistula inahitaji ujasiri na wadau wa afaya kushiriki ambapo pia amesema CCBRT inashirikiana na  mfuko wa Umoja wa Mataifa wa idadi ya watu UNFPA.