Turejeshe mamlaka ya taifa la Mali kwa amani ya nchi: Ladsous

Turejeshe mamlaka ya taifa la Mali kwa amani ya nchi: Ladsous

Lazima taifa la Mali lirudishiwe mamlaka yake tena ili kulinusuru katika mgogoro unaondelea amesema mkuu wa  operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa Herve Ladsous wakati akihutubia baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lililojadili hali nchini humo.

Ladsous amesema licha ya kwamba kazi ya ulinzi wa amani nchini humo inakumbana na changamoto mbalimbali ikiwamo matukio kadhaa ya kushambuliwa kwa walinda amani, kazi ya kurejesha amani inasali jukumu muhimu.

Akitolea mfano amesema hivi karibuni walinzi wa amani wakiwa katika operesheni zao za amani walishambuliwa na kujeruhiwa.

Kwa upande wake mwakilishi wa kudumu wa Mali katika Umoja wa Mataifa   Sékou Kassé,  amesema ni vizuri ahadi za makubaliano ya amani yaliyofikiwa mwaka 2014 zikaheshimiwa ili kufikia amani ya kweli.