Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Amos kutembelea Lebanon kujionea hali halisi ya kibinadamu

Amos kutembelea Lebanon kujionea hali halisi ya kibinadamu

Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloratibu misaada ya kibinadamu, OCHA, Bi. Valeri Amos anatarajiwa kutembelea Lebanon kuanzia tarehe 7 hadi 9 January.

Wakati wa ziara yake, Bi Amos anatarajiwa kukutana na viongozi waandamizi wa Lebanon, wakuu wa serikali za mitaa, washirika wa kibinaadamu na watu walioathirika na mgogoro unaoendelea ya Syria.

Halikadhalika, ziara yake pia inatathmini jinsi jumuiya ya kimataifa inavyoweza kusaidia serikali ya Lebanon kutoa msaada kwa raia wa Lebanon, Wasyria na Wapalestina wanaoshi katika mazingira magumu.

Mpango uliozinduliwa hivi karibuni wa kukabiliana na mgogoro wa Lebanon umebaini kuwa takriban watu milioni 2.2 wanaoishi katika  mazingira magumu, wengi wao wakiwa ni wakimbizi kutoka Syria  wanahitaji misaada ya kibinadamu na ulinzi.