Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Udongo wenye afya ni msingi wa afya :FAO

Udongo wenye afya ni msingi wa afya :FAO

Rutuba ya udongo iko katika hatari ya kudidimia kwa sababu mbali mbali ikiwemo kuimarika kwa miji, ukataji miti, matumizi mabaya ya ardhi, uchafuzi  wa mazingira, na mabadiliko ya tabianchi .

Uharibifu wa rutuba ya udongo unatishia uwezo wa  kutimiza mahitaji ya vizazi vijavyo . Hii ni kwa mujibu wa Shirika la kilimo duniani FAO katika mwaka wa maadhimisho ya udongo 2015.

Kauli mbiu ya mwaka huu wa udongo ni: udongo wenye afya kwa maisha yenye afya ambapo FAO inasema kwamba iwapo udongo utakuwa katika hatari ya kuharibiwa , maendeleo endelevu ya kilimo, usalama wa chakula na mazingira kamilifu yako hatarini.

Ili kupunguza uharibifu wa udongo Dr. James Mutegi ambaye ni mtaalamu wa afya ya udongo kutoka taasisi ya afya ya udongo ya kimataifa nchini Kenya anashauri...

(Sauti ya Dkt Mutegi )