Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNRWA yakaribisha uteuzi wa Naibu Kamishna Mkuu

UNRWA yakaribisha uteuzi wa Naibu Kamishna Mkuu

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Palestina, UNRWA limekaribisha uteuzi wa Naibu Kamishna mkuu wa UNRWA  Sandra Mitchell .

Bi Mitchell ambaye ameteuliwa na Katibu Mkuu wa UM anachukua nafasi ya Margot Ellis.

Katibu Mkuu na Kamishna Mkuu wa UNRWA, Pierre Krähenbühl wamemshukuru Bi Ellis kwa huduma ya kujitolea kwa wakimbizi wa Palestina kwa zaidi ya miaka mitano iliyopita haswa uongozi wake katika kutekeleza mamlaka ya UNRWA Syria.

Bi Mitchell anauzoefu wa uongozi wa ngazi za juu ambapo pia amewahi kuhudumu nafasi ya makamu wa Rais wa Kamati ya Kimataifa ya Uokozi.