Mgogoro wa Syria watoa fursa finyu kwa elimu ya watoto : UNICEF

6 Januari 2015

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, limesema mgogoro unaoendelea nchini Syria kwa miaka mitano mfululizo umesababisha kuuawa kwa takribani watoto 160 huku wengine 343 wakijeruhiwa mwaka jana. Taarifa kamili na Amina Hassan.

(TAARIFA YA AMINA)

Mwakilishi wa UNICEF nchini Syria, Hanaa Singer amesema mbali na ukosefu wa shule, mashambulizi dhidi ya shule, walimu na wanafunzi ni ishara tosha ya madhila ya mgogoro huo kwa watoto.

Kwa mujibu wa UNICEF kufungwa kwa shule hivi karibuni katika majimbo ya Raqqa na Deir-ez-Zour na maeneo ya vijijini mjini Aleppo, kumevuruga elimu kwa watoto 670,000 wenye umri wa kwenda shule za msingi na za sekondari.

Singer amesema upatikanaji wa elimu ni haki kwa watoto wote, bila kujali wanapoishi au ugumu wa mazingira yao haswa wakati huu wa mgogoro wa kutisha.

Christophe Boulierac ni msemaji wa UNICEF..

"Kulikuwa na baadhi ya ripoti kwamba kundi linalotaka kuweka dola la kiislamu lilitaka kubadili mitaaka ya shule. Hiyo ni mojawapo ya sababu, bila shaka sababu nyingine ya shule kufungwa ni ya kiusalama baada ya mashambulizi. Lakini ukweli ni kwamba kundi linalotaka kuweka dola la Kiislamu lilitaka mtaala ifanyiwe mapinduzi au ibuniwe upya ndio maana baadhi ya shule zilifungwa."

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter