Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kampeni dhidi ya Fistula, CCBRT yaonyesha mfano

Kampeni dhidi ya Fistula, CCBRT yaonyesha mfano

Wakati wa malengo ya maendeleo ya milenia yakifikia ukomo mwaka huu wa 2015 Umoja wa Mataifa kupitia baraza kuu umetaka kukomeshwa kwa fistula ugonjwa unaowakumba wanawake kutokana na kukosa huduma mujarabu wakati wa kujifungua.

Kupitia azimio lililopitishwa na baraza kuu, umoja huo unataka hatua zichukuliwe na wadau wa afya ili kunusuru wanawake milioni 2 kote duniani wanaokadiriwa kuuguwa Fistula aina ya obstetric ambapo mfuko wa Umoja wa Mataifa wa idadi ya watu UNFPA umetaka jumuiya ya kimataifa kusaidia wanawake wajawazito na kupambana na Fistula kwa nguvu zaidi.

Miongoni mwa taasisi zinazosaidia wanawake wenye Fistula ni shirika lisilo la kiserikali la afya CCBRT nchini Tanzania ambapo meneja mawasiliano Abdul Kajumuo anaeleza wanachofanya

(SAUTI KAJUMULO)