Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uturuki ndio mfano wa kuigwa wa diplomasia kwa sasa:Bokova

Uturuki ndio mfano wa kuigwa wa diplomasia kwa sasa:Bokova

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO , Irina Bokova amesema mila ya Uturuki ndio umbo wa diplomasia kama tunavyojua hivi sasa.

Katika hotuba yake wakati wa Mkutano wa Saba wa kila mwaka wa mabalozi mjini Ankara Bi Bukova alisifu Uturuki kama kiongozi mashuhuri wa kiuchumi na sauti kimataifa.

Akitolea mfano, Bokova amesema Uturuki sasa inasimamia G20, jukwaa la kimataifa kwa serikali na magavana wa benki kuu kutoka uchumi kubwa 20 duniani.

Aidha, Bi Bokova amesema anatarajia kuimarisha ushirikiano wa Uturuki na UNESCO.