Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chile yachukua Urais wa Baraza la Usalama kwa mwezi wa Januari

Chile yachukua Urais wa Baraza la Usalama kwa mwezi wa Januari

Wanachama watano wapya wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wanatarajiwa kuhudhuria mkutano wa Baraza hilo kwa mara ya kwanza mwaka huu. wakati taifa la Amerika Kusini, Chile likishikilia Urais wa Baraza la Usalama la kwa mwezi wa Januari mwaka huu.

Angola, Malaysia, New Zealand,Uhispania na Venezuela ni wanachama wapya wasio wa kudumu na wote wanatumikia kipindi cha miaka miwili.Balozi wa Chile katika Umoja wa Mataifa, Cristian Barros Melet anaelezea madhumuni ya mjadala wa wazi wa Baraza hilo ambayo utakuwa chini ya uenyekiti wa Rais wa Chile, Michelle Bachelet hapo Januari 19.

Ni matumaini yetu kwamba mjadala huu utachangia katika njia ya kina ya maendeleo shirikishi, kwa wigo mpana kadri iwezekanavyo, ambapo itahusisha kuzuia vita na kujenga amani. Ni matumaini yetu lengo la mjadala huu utachagiza juhudi itakayoboresha hatua ya Baraza litaridhia ikizingatiwa vitisho viwili”