Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Juhudi za majadiliano Libya zinaendelea:UNSMIL

Juhudi za majadiliano Libya zinaendelea:UNSMIL

Majadiliano yanaendelea miongoni mwa wanasiasa wa Libya kuhusu awamu ya pili ya mazungumzo ya amani amesema msemaji wa Umoja wa Mataifa.Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa usaidizi nchini Libya UNSMIL , umekuwa ukiunga mkono majadiliano kama njia ya kusitisha mgogoro wa kisiasa na kiusalama nchini humo

Mazungumzo yaliyokuwa yamepangwa kufanyika mnamo Disemba 9 yalikatizwa kufuatia hali tete nchini humo

Raia wa Libya wanakimbia mapigano kati ya makundi kinzani yenye silaha mijini ikiwamo pia mashmbulizi ya anga yanayoelekezwa mjini Misrata.

Samir Ghattas wa UNSMIL anasema mazungumzo yanakabiliana na changamoto.

"Moja ya changamoto kuu kwatu pia ni eneo la kukutania. Akama unavyofahamu Umoja wa Mataifa una mahitaji yake ya ulinzi na tunataka kuhakikisha pande zote wanakubali eneo la kukutana. Hilo ni moja, jingine ni majira muafaka. Masuala mengine yanahusiana na ajenda na siasa za Libya ambazo ni ngumu sana."  

Libya imeingia katika mzozo tangu kuondolewa madarakani kwa aliyekuwa kiongozi wake  Muammar al-Qhadafi  takribani miaka mitano iliyopita.