Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ILO yataka kampuni za kimataifa kuheshimu ongezekeo la mishahara Cambodia

ILO yataka kampuni za kimataifa kuheshimu ongezekeo la mishahara Cambodia

Kampuni za nguo za kimataifa ambazo zinanunua bidhaa zao nchini Cambodia zinapaswa kusaidia kampuni za Cambodia kukabiliana na ongezeko la kima cha chini cha mshahara, kwa mujibu wa wataalamu wa Shirika la Kazi duniani, ILO.

Kima cha chini cha mshahara kimeongezeka kutoka kwa dola 183 kwa mwezi hadi dola 217. Hii ni kwa zaidi ya watu laki tano Cambodia.

Matokeo yanayotarajiwa ni kuongezeka kwa gharama za kutengeneza nguo na bidhaa nyingine kwa asilimia 18 na kupungua kwa faida ya kampuni za Cambodia.

Mkurugenzi wa ILO nchini Cambodia ameziomba kampuni za nje kuongeza bei za bidhaa wanazonunua kutoka Cambodia ili kusaidia kampuni za Cambodia kukabiliana na gharama hizo mpya.