Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtalaam maalum wa UM kufanya ziara kutathimini haki za binadamu Myanmar

Mtalaam maalum wa UM kufanya ziara kutathimini haki za binadamu Myanmar

Mtalaam maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Mynmar Yanghee Lee atafanya ziara yake ya pili nchini humo kuanzia tarehe 7 hadi 16 Januari mwaka huu kwa ajili ya kutathmini hali ya kibinadamu ilivyo katika jimbo la Rakhine na Shan kaskazini . Priscilla Lecomte ana maelezo kamili

(TAARIFA YA PRISCILLA)

Bi Lee amesema kwamba atatembelea kambi za wakimbizi wa ndani katika maeneo yaliotengwa katika jimbo la Rakhine ili kutathmini kama hali imeimarika tangu ziara yake ya kwanza mnamo Julai 2014.

Katika jimbo la kaskazini la Shan mtaalam huyo ataangazia hali ya kidini na kikabila kwa makundi madogo madogo. Aidha atazungumzia kuhusu maswala ya ukatili wa kijinsia kwa kuzingatia mzozo unaoshuhudiwa katika eneo hilo.

Kadhalika bi Lee ameelezea wasiwasi wake kuhusu kupitishwa kwa miswada kuhusu ulinzi wa watu kwa misingi ya rangi na dini ambayo ina vipengele ambavyo havitimizi vigezo vya haki za binadamu za kimataifa. Kwa mujibu wa Bi Lee iwapo miswada hiyo itapitishwa huenda ikahalalisha ubaguzi wa kidini na makabila ya watu walio wachache na wanawake.