Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu mpya wa UNMEER aanza kazi rasmi

Mkuu mpya wa UNMEER aanza kazi rasmi

Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kushughulikia dharura ya Ebola, UNMEER, Ismail Ould Cheikh Ahmed ameanza majukumu yake jumamosi tarehe 3, januari, baada ya kuchukua nafasi ya mkuu wa zamani, Anthony Banbury.

Bwana Ahmed, wakati wa mkutano uliofanyika mjini Accra, Ghana amepongeza mafanikio ya kila mshirika katika kukabiliana na Ebola, akibainisha kuwa bado kuna kazi kubwa ya kufanywa.
Taarifa kutoka ujumbe wa UNMEER imesema kwamba Ould Cheikh Ahmed atatembelea Guinea, Liberia na Sierra Leone wiki ijayo ili kuimarisha mikakati ya UNMEER na kushuhudia mwenyewe hali halisi ya vita dhidi ya Ebola.
Msaada wa UNMEER na wadau wengine umesaidia nchi za Guinea, Liberia na Sierra Leone ili kufikia malengo yaliyowekwa ya kutenga asilimia 100 ya wagonjwa wa Ebola, kutibu asilimia 100 ya visa vilivyothibitishwa na Ebola na kuzika asilimia 100 ya watu waliokufa na Ebola kwa usalama na heshima.