Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Harakati za wanawake kujikwamua kiuchumi

Harakati za wanawake kujikwamua kiuchumi

Lengo namba tatu la maendeleo ya milenia yanayofikia ukomo wake mwaka huu ni usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake. Lengo hili linataka wanawake wapewe fursa sawa katika nyanja zote ikiwamo kiuchumi, kisiasa na hata kijamii.

Katika Umoja wa Mataifa shirika linalojihusisha na maslahi ya kundi hilo, UN Women limekuwa mstari wa mbele kuhakikisha wanawake wanawezeshwa katika nyanja zote. Mathalani shirika hili kupitia kwa Mwenyekiti wake Pumzile Mlambo Ncguka linataka mwaka huu wa 2015 uwe mwaka ambao dunia itajielekeza kuhakikisha wanawake wanapewa kipaumbele katika msukumo wa maendeleo na kuondokana na dhuluma zinazokandamiza kundi hilo. Nchini Tanzania wanawake wako mstari wa mbele katika kujikwamua kiuchumi na hivyo kuondokana na dhana ya utegemezi.

Miongoni mwao ni Rose Matu, mama mjasiriamali anayemiliki shule ya awali, anayefuga kuku na kujishughulisha na upishi. Paulina Mpiwa wa radio washirika Sengrema Fm amemtembelea bi Rose katika banda lake la kuku, ungana naye.