Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wajumbe wa kimataifa wa Ukanda wa Maziwa Makuu watoa wito dhidi ya FDLR

Wajumbe wa kimataifa wa Ukanda wa Maziwa Makuu watoa wito dhidi ya FDLR

Leo ndio siku ya mwisho ya kipindi cha miezi sita iliyotolewa na  taasisi za kikanda ikiwemo mkutano wa kimataifa wa maziwa makuu, ICGLR na  nchi za kusini mwa Afrika, SADC  ya kujisalimisha kamili na bila masharti kwa kundi la waasi la FDLR nchni Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, DRC.

Katika taarifa, timu ya Kimataifa ya Wajumbe, wakiwemo Mjumbe Maalum wa maziwa makuu, Said Djinnit, mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa na mkuu wa MONUSCO, Martin Kobler, Mwakilishi Maalum wa Muungano wa Afrika katika Maziwa Makuu, Boubacar Diarra, Mratibu wa Muungano wa Ulaya katika Maziwa Makuu, Koen Vervaeke, mjumbe maalum wa serikali ya Marekani katika maziwa Makuu na DRC, Russell Feingold D. na mjumbe Maalum kwa ajili ya Maziwa Makuu wa Ubelgiji, Frank de Coninck, wameelezea wasiwasi wao kwamba kundi la FDLR halijatimza amri hiyo.

Wajumbe hao walisema, badala yake, FDLR imetumia kipindi hicho cha miezi sita kuendelea kufanya ukiukwaji wa haki za binadamu dhidi ya watu wasio na hatia katika Mashariki mwa DRC, kuwaajiri wapiganaji, na kutetea ajenda yao haramu ya kisiasa.

Kwa ujibu wa viongozi hao , kukomesha tishio la FDLR si wajibu DRC pekee, bali ni wajibu wa kikanda na kimataifa.