Mkutano wa tahadhari dhidi ya Tsunami kufanyika Japan

2 Januari 2015

Tetemeko la ardhi chini ya bahari la Tsunami la  mwaka wa 2004 limekuwa kichochezi cha kuundwa kwa Mfumo wa Hyogo ambao ni  mkataba wa kimataifa waa kupunguza hatari itokanyo na maafa. Abdullahi Boru na maelzeo zaidi.

(TAARIFA YA ABDULLAHI)

Maadhimisho ya mwongo mmoja baada ya janga hilo la Tsunami, imesababisha kutolewa kwa wito wa kasi ya makubaliano sawia wa mustakbali wa kurejea katika maisha ya kawaida baada ya janga , ambao utajadiliwa wakati wa mkutano wa tatuu wa kupunguza hatari zitokanazo na majanga mwezi March mwaka huu katika mji wa Sendai nchini Japan.

Makumbusho ya Tsunami yalitoa fursa ya wazi ya mshtuko wa dunia baada ya maafa hayo ambapo zaisi ya watu 200,000 walipoteza maisha yao na kuchagiza juhudi za kimataifa za usaidizi kwa jamii zilizothiriwa.

Halikadhalika , kuelekea tukio hilo,  Ofisi ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Kupunguza Maafa Hatari , UNISDR,imekuwa ikifanya kazi kwa kushirikiana na serikali ya Thailand ili kutathmini mafunzo mwafaka kutokana na janga hilo kwa kufanya mkutano na washikadau kama viongozi wa kikanda na wakuu wa sekta ya biashara.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud