Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Udongo wenye rutuba ni msingi wa kilimo na afya na unapaswa kutunzwa

Udongo wenye rutuba ni msingi wa kilimo na afya na unapaswa kutunzwa

Jarida letu maalum leo linaangazia mwaka wa udongo 2015.Mwaka huu umetajwa kama mwaka wa kuchagiza hatua za kulinda rutuba ya udongo ambayo inaendelea kudidimia kutokana na sababu za kiasili na pia za kibinadamu. Udongo wenye rutuba ndio msingi wa mimea na kilimo. Misitu inahitaji udongo wenye rutuba na sisi tunahitaji udongo huo kwa ajili ya chakula, lishe ya mifugo, baioanuai na mengine mengi. Hayo ni kulingana na Mkurugenzi Mkuu wa shirika la chakula na kilimo duniani, FAO José Graziano da Silva wakati wa uzinduzi wa mwaka wa udongo.FAO inasema kutokana na umuhimu huo ni vyema kuepuka uharibifu wa mazingira unaotishia udongo wenye rutuba kwa kuwa uzalishaji wa chakula kwa watu zaidi ya Milioni 805 wenye njaa duniani kote utakuwa mashakani.Bara la Afrika ndilo linashuhudia ukosefu wa usalama wa chakula, Nchini Kenya moja ya nchi ambazo zinategemea kilimo kama uti wa uchumi wa nchi hali ikoje? Geoffrey Onditi wa radio washirika wa Shirika la utangazaji KBC ametuandalia ripoti ifuatayo.

(Studio Pkg)