Baraza la Usalama lakataa azimio la kumaliza ukazi wa Palestina na Israel

31 Disemba 2014

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekataa rasimu ya azimio ya kumaliza ukalizi wa eneo la Palestina na Israeili kufikia mwaka wa 2017.

Wakati wa kupigwa kura baraza hilo lenye wanachama 15 liligawanyika wakati wanachama nane wakiunga mkono azimio hilo huku Marekani na Australia ikipinga.Mataifa matano hayakupiga kura.

Kwa kawaida, theluti mbili za kura zinahitaji ili kupitishwa kwa azimio kama hilo mradi taifa lilo na kura ya turufu lisipinge.

Mapema mwezi huu, Jordan iliwasilisha pendekezo ambalo katika miezi kumi na miwili ya ukalizi wa eneo la Palestina na Israel utamalizika katika kile Jordan ilichokitaja kama uvamizi wa Israel tangu mwaka 1967.

Halikadhalika, rasimu ya azimio hilo ilipendekeza pia kujenga mataifa mawili huru na ya kidemokrasia yaani Israel na Palestina.

Mwakilishi wa Kudumu wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Samantha Power, alieleza ni kwa nini nchi yake ilipiga kura dhidi ya azimio hilo .

“Kwa bahati mbaya, badala ya kutoa sauti na matarajio ya Wapelestina na Israel, Nakala hii inaangazia wasiwasi wa upande mmoja tu. Inausawa wa kindani na ina mambo mengi ambayo si mazuri kwa mazungumzo kati ya pande zote ikiwa ni pamoja na muda usiofaa ambayo haizingatii masuala halali ya usalama wa Israeli”.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter