Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Migogoro mingine iliojiri Afrika

Migogoro mingine iliojiri Afrika

Kwingineko, Mzozo wa Syria bado unaendelea ukiingia mwaka wa tatu .Mgogoro huu umechukua sura mpya baada ya kuibuka kwa makundi ya dola la uislamu wenye msimamo mkali ISIL kundi ambalo pia linachukua kasi pia nchini Iraq.

Juhudi za Umoja wa Mataifa za katufuta ufumbuzi wa kisiasa nchini Iraq na Syria pamoja na kushughulikia mahitaji ya kibinidamu zinaendeela katiak migogoro hiyo inayovuka mipaka.

Nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR hali bado ni tete huku jamii hasimu zikizidi kukinzana. Kwa upande wake, UM mnamo mwezi April mwaka huu umedhihiridha adhma ya ke ya kutafuta amani ya kudumu CAR, kwa kuunda Ujumbe wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, MINUSCA . Mojawapo ya mamlaka ya Ujumbe huo ni kuhifadhi utawala wa serikali ya nchi hiyo na raia.

Hatimaye, nchini Sudan Kusini bado machafuko yanayotokana na mvutano baina ya wapiganajai wanaomuunga mkono Rais Salva Kir na wale wampinzani wake Riek Macahr yanaendelea.

Mustakabili wa wakimbizi kufuatia machafuko hayo unategemea matokeo ya mazungumza ya amani yanayoendelea huku Addis Ababa Ethiopia.