Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ebola yatikisa Dunia mwaka 2014

Ebola yatikisa Dunia mwaka 2014

Mwaka wa 2014 mlipuko mkubwa zaidi kuwahi kutokea wa Ebola ulizuka huko Afrika Magharibi huku ukiwauwa zaidi ya watu 7500 huku visa 19 497 vikiripotiwa  na kuathiri maisha ya maelfu ya watu.

Mkurugenzi Mkuu wa WHO Margaret Chan alitaja mlipuko wa homa ya ebola kama mzozo wa kijamii, kibinadamu, kiuchumi na tishio kwa usalama wa kitaifa na nje ya mipaka ya Afrika Magharibi unakoshuhudiwa kwani visa vya ebola viligunduliwa katika baadhi ya nchi ikiwemo Nigeria, Senegal, Uhispania na Marekani.  Baadhi ya nchi zinazokabiliwa na mlipuko huo ni, Sierra Leone, Guinea, Mali na Liberia ambako ndiko kulitikiswa zaidi wakati wa mlipuko wa homa kali ya ebola kugunduliwa. Je hali ikoje kwa sasa Kamanda Mkuu wa vikosi vya ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Liberia UNMIL, Meja Jenerali Leonard Ngondi anaeleza

(NGONDI EBOLA CLIP)

Kwa sasa ripoti zinasema kwamba ni 70% ya vifo ndani ya visa vyote vinavyoripotiwa.