Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Matumaini ya Afrika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ni hafifu: Mtaalamu

Matumaini ya Afrika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ni hafifu: Mtaalamu

Mabadiliko ya tabia nchi imekuwa miongoni mwa ajenda kuu za Umoja wa Mataifa na jumuiya ya kimataifa  kwa mwaka 2014.

Katibu Mkuu Ban Ki- Moon amekuwa mstari wa mbele kupigia upatu suala hili na kuratibu mkutano uliowaleta pamoja viongozi wa nchi wanachama wa UM wakati wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa hapa New York. Mkutano ulijadili namna ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi pamoja na kila nchi kueleza inachofanya katika kukabiliana na janga hilo.

Kutoka  New York hadi Peru Lima, ni mkutano wa ishirini wa mabadiliko ya tabia nchi  COP20 ambapo ufikiwaji wa mkataba wa kimataifa wa masuala ya mabadiliko ya tabia nchi ulijadiliwa. Mkataba huo unatarajiwa kukamilishwa katika mkutano wa Paris mwaka 2015.

Miongoni mwa yaliyofikiwa katika COP 20 Peru ni kupitishwa kwa nyaraka iitwayo Wito wa Lima kwa hatua kuhusu tabianchi.

Pia washiriki wametoa ahadi za kutekeleza ikiwemo hatua watakazochukua kupunguza utoaji wa hewa chafuzi na kuzuia vitendo vya kibinadamu vinavyoathiri sayari ya duniaNini matumaini ya Afrika bara lililoshuhudia madhara ya mabailiko ya tabia nchi. Dk Julius Ningu ni mtaalamu wa mazingira na mkurugenzi wa mazingira katika ofisi ya makamau wa Rais wa Tanzania

(SAUTI DK NINGU)