Makao makuu ya UN mbioni kukarabatiwa

Makao makuu ya UN mbioni kukarabatiwa

Hatimaye makao makuu ya Umoja ya Ofisi za Umoja wa Mataifa yaliyoko barani Ulaya sasa yataanza kukarabatiwa wakati wowote kuanzia sasa kufuatia nchi wanachama kukubali kutenga fedha kwa ajili ya kufanikisha mpango huo.

Kukubaliwa kwa ombi hilo kunafuatia onyo lililotolewa na Naibu Mwakilishi Uswis katika Umoja wa Mataifa Olivier Zehnder aliyesema kuwa ‘ukarabati wa majengo hayo ni jambo lisilokwepeka’.

Nchi hizo wanachama zimekubaliana kutenga kiasi cha Dola za Marekani milioni 28 kwa ajili ya kuanzisha mpango huo wa ukarabati. Ukarabati wa majengo hayo yaliyoko mjini Geneva unakadiriwa kufikia kiasi cha Dola za Marekani milioni 850.