Msaada wa Uturuki kwa Gaza hatimaye wawasili

31 Disemba 2014

Msafara wa mwisho wa meli iliyobeBa unga wa ngano uliotolewa na Serikali ya Uturuki kwa ajili ya Gaza umetia nanga hii leo katika eneo la ufukwe wa Palestina.

Kiasi hicho cha unga chenye thamani ya Dola za Marekani milioni 6.25 kinatazamiwa kuzinufaisga zaidi ya familia 140,000 katika eneo hilo la Ukanda wa Gaza.

Naibu Kamishna wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Palestina  UNRWA Margot Ellis  amesema mapigano ya hivi karibuni pamoja na vikwazo vya miaka mingi vimevuruga kabisa hali ya uchumi wa Gaza.

Bwana Ellis amesema kuwa kutolewa kwa msaada huo ni habari njema kwa wakazi wa eneo hilo na kwamba familia nyingi sasa zitapata unafuu wa maisha.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter