Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNRWA yatoa mafunzo kwa wanafunzi wakimbizi kutengeza bidhaa kwa taka

UNRWA yatoa mafunzo kwa wanafunzi wakimbizi kutengeza bidhaa kwa taka

Wanafunzi waliofurushwa makwao kufuatia mapigano yaliyodumu kwa miaka minne huko nchini Syria wananufaika na mafunzo yanotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi wa Palestina UNRWA, ya kutegenza bidhaa kwa kutumia taka.

Wanafunzi kumi na wawili wamejiunga na kozi hiyo ya miezi miwili iliyofanyika katika kituo cha mafunzo cha URNWA na kinaangazia kazi ya mikono mathalani kufuma na kusuka vikapu.

Kwa mujibu wa UNRWA, kozi hiyo inaweza kugeuza uzeufu wao mgumu ya kufurushwa makwao kuwa vichocheo vya kupata ujuzi wa kazi mpya na maisha mapya.

Wanafunzi walikuwa wanatumia mfuko wa plastiki, karatasi, magazeti na makopo tupu ili kutengeneza vitu vilivyo na manufaa kama vile viti na shada la taa za kuni’ingi’inia.

Mfunzo hayo yamefadhiliwa na Muungano wa Ulaya.