Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNSMIL yalaani shambulizi la kigaidi nchini Libya

UNSMIL yalaani shambulizi la kigaidi nchini Libya

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya, UNSMIL umelaani shambulizi la kigaidi lilolenga hoteli katika mji wa Tobruk nchini Libya.

Wakati was shambulizi hilo baraza la wawakilishi la Libya lilikuwa likifanya kikao chake katika hoteli hiyo ilioko karibu na mpaka wa Misri.

Taarifa za vyombo vya habari nchini Libya zimesema mshambuliaji wa kujitoa mhanga alilipua gari lilokuwa na bomu ambapo watu watatu walijeruhiwa.UNSMIL imesema shambulizi hilo litaongeza tu ari ya wale wanaotaka kupatikana kwa ufumbuzi wa kisiasa na kusonesha juhudi za kuleta utulivu na usalama nchini Libya.

Tangu kutimuliwa kwa Muammar al-Qhadafi mamlakani 2010 Libya imekumbwa na migogoro.