Hali ya haki za binadamu Bahrain inasikikitisha

30 Disemba 2014

Ofisi ya Haki za Binadamu  Umoja wa Mataifa imeelezea wasiwasi wake kuhusu kukamatwa kwa kiongozi wa kikundi cha harakati za upinzani  cha Al Wefaq, Sheikh Ali Salman, na unyanyasaji na kuweka korokoroni kwa watu wanaotekeleza haki zao za uhuru wa maoni na kujieleza. Taarifa zaidi na Joseph Msami

(TAARIFA YA MSAMI)

Katika taarifa yake , ofisi hiyo imesema  taarifa za kuaminika zilizokusanywa na Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa huko Geneva, Sheikh Salman alikamatwa baada ya kuitwa kwa mahojiano katika Idara ya Upelelezi wa makosa ya jinai siku ya jumapili, siku mbili tu baada yake kuchaguliwa  kwa kipindi cha nne kama Katibu Mkuu wa Al Wefaq .

Wakili wake wamesema anakabiliwa na mashtaka makubwa ambayo yanaweza kumuweka gerezani kwa kipindi kirefu ikiwa ni pamoja na wito wa kupindua serikali.

Kwa maantikia hiyo, Ofisi za Haki za Binadamu imieomba serikali ya Bahrain kumwachilia Shekh Salman na wale wote waliowekwa kizuizini  kwa ajili ya kutekeleza haki yao ya msingi ya uhuru wa kujieleza na kukusanyika.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter