Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wilaya ya Kailahun nchini Sierra Leone yadhibiti Ebola

Wilaya ya Kailahun nchini Sierra Leone yadhibiti Ebola

Wilaya ya Kailahun mashariki mwa Sierra Leone ni eneo la kwanza ambapo ugonjwa wa Ebola ulizuka, wakati wa kilele cha maambukizi, Visa zaidi ya  80 vikiripotiwa kila siku hadi mwishoni mwa mwezi Juni 2014. Sasa ugonjwa huo umedhibitiwa wilayani hapo

Kwa msaada wa Shirika la afya duniani, WHO na washirika, pamoja na ushiriki wa karibu wa viongozi  kijamii, wilaya hiyo iliweza kudhibiti Ebola, na kwa wiki kadhaa hakuna visa vipya.

Licha ya mafanikio hayo, timu ya wafanyakazi wa afya wako katika hali ya tahadhari ya juu ili kukabiliana haraka na maambukizi yoyote mapya haraka iwezekanavyo.

Dk Zabuloni Yoti, kiongozi wa timu ya WHO ambaye anauzoefu wa kukabiliana na homa kama Ebola amesema wakati alipowasili mwezi wa juni maambukizi ya Ebola bado yalikuwa katika eneo la Kailahun, na kwamba kulikiwa na upinzani mkali kutoka kwa jamii huku baadhi yao wakiwazuia timu yake kutembelea maeneo fulani lakini ujenzi wa uhusiano na viongozi wa jamii ukawezesha kutokomeza Ebola.