Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtambo wa ukoaji sasa wasambazwa Phunket kukabili tsunami

UN Photo/Evan Schneider
Picha:

Mtambo wa ukoaji sasa wasambazwa Phunket kukabili tsunami

Mwongo mmoja tangu kuzuka kwa tetemeko la chini ya bahari, Tsunami katika baadhi ya nchi za Asia hivi sasa kuna hatua kubwa zilizopigwa ikiwamo kuweka kwa mitambo inayotoa tahadhari ya mapema.

Mtambo uliowekwa kwenye fukwe ya Phunket unatajwa kuwa ni tahadhari kubwa iliyochukuliwa katika eneo hilo kwa ajili ya kuwalinda wananchi pamoja na watalii mbalimbali wanamiminika mara kwa mara.

Mtambo huo unaojulikana kama Le Meridien  umeunganishwa katika migahawa mbalimbali duniani kwa ajili ya kutoa taarifa za mapema pindi janga lolote linapojitokeza.

Mtambo huo unatoa mwongozo na maelekezo ya nini cha kufanya wakati wa tukio lolote la dharura linalojitokeza katika maeneo ya pwani.