Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN yaalani mashambulizi ya anga Libya

Nyumba iliyoharibiwa Ahy Badr katika mji wa Mizdah kwenye milima ya Nafusa Libya baada ya vita vya kikabila Machi 2013. Picha: IRIN / Jorge Vitoria Rubio(UN News Centre)

UN yaalani mashambulizi ya anga Libya

Umoja wa Mataifa umelaani vikali tukio la mashambulizi ya anga yaliyofanywa mwishoni mwa wiki katika mji wa Misrata nchini Libya na kusababisha madhara kwa raia.

Katika taarifa yake, Kamishna ya UN kwa ajili ya Libya UNSIMIL umezitaka pande zote zinazohusika katika mzozo wa Libya kujiepusha na matukio yanayoweza kulirudisha upya taifa hilo kwenye mapigano.

UN imesisitiza kuwa hatua yoyote ya kuchochea mapigano inaweza kuitumbukiza Libya katika hali mbaya zaidi na hivyo kusababisha kukosekana kwa amani ya kudumu.