29 Disemba 2014
Watumishi wanaofanya kazi za usamaria mwema duniani kote wamepongezwa kutokana na mchango wao hasa kwa kushiriki kufanya kazi katika mazingira hatarishi na yenye kuleta hali ya wasiwasi.
Pongezi hizo zilitolewa na maofisa wa ngazi za juu za Umoja wa Mataifa zimezingatia pia ripoti za hivi karibuni ambazo zimewatambua wafanyakazi55 waliopoteza maisha wakati wakiwa kwenye operesheni zao.
Baadhi yao walipoteza maisha katika nchi za Syria, Afghanistan na Sudan Kusini. Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na misaada ya dharura OCHA, John Ging amesema kuwa pamoja na hali ngumu zinazowaandama wafanyakazi hao lakini bado wameendelea kuonyesha utu wao kwa kuchapa kazi bila woga.