Bahrain inakandamiza watetezi wa haki za binadamu wanawake

29 Disemba 2014

Watalaalamu wa  Umoja wa Mataifa juu ya haki za binadamu wameitaka Bahrain kuondosha mashtaka yanayowakabili wanawake ambao wamekuwa mstari wa mbele kwa ukosoaji wa serikali inayolalamikiwa  kwa kukiuka haki za binadamu. Taarifa kamili na George Njogopa.

(Sauti ya George)

Jopo hilo la wataalamu limesema kuwa serikali ya Bahrain inapaswa kuyaondosha mashtaka yanayowakabili wanawake watatu ambao wamekuwa wakiandamwa na dola kutokana na misimamo yao ya kupigania na kutetea haki za binadamu.

Hivi karibuni mahakama ya Bahrain iliwatia korokoroni wanawake hao akiwamo Mkurugunzi msaadizi wa kituo cha kutetea haki za binadamu katika eneo la Ghuba Maryam Al-Khawaja kwa madai ya shambulio dhidi ya mwanausalama mmoja wa uwanja wa ndege. Hata hivyo wakati hukumu hiyo ikitolewa Maryam alikuwa nje ya nchi.

Mwingine aliyetupwa gerezani ni mwanaharakati  Zainab Al-Khawaja ambaye ni ndugu na Maryam. Yeye amehukumiwa kwenda jela miaka mitatu kwa kosa la kuchana picha ya Mfalme . Pia anakabiliwa na makosa mengine.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter