Maadhimisho ya Miaka Sabini ya Umoja wa Mataifa, tukumbuke mafanikio ya UM: UNDP

29 Disemba 2014

Tukiwa tunaelekea maadhimisho ya miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa imeelezwa kuwa miongoni mwa mafanikio yaliyotekelezwa na umoja huo ni kutokomeza magonjwa duniani ikiwamo ule wa ndui.

Katika mahojiano na Derick Mbatha wa Idhaa ya Kingereza ya UM Naibu Mkurugenzi wa Ushirikiano na Umma katika Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa, UNDP, Ramu Damodaran, amesema maadhimisho ya miaka 70 ni nafasi ya kuangalia na  kuzingatia mafanikio ya Umoja wa Mataifa mathalani  katika sekta ya afya.

 “Tunapofikiria jinsi Ebola inavyosambaa na kuthibitiwa, akili zetu zinarudi nyuma wakati katika karne ya 20 ambapo karibu watu millioni 500 walikuwa wameambukizwa Ndui. Na kwa sababu ya Umoja huu , na kwa sababu ya vipaji vya kimatibabu na vya Kibinadamu , ugonjwa wa Ndui, ulitokomezwa mwaka wa 1975”

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter