Banbury aanza ziara ya mwisho Afrika Magharibi, awasili Liberia leo

29 Disemba 2014

Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kushughulikia dharura ya Ebola UNMEER  Anthony Banbury anawasili nchini Liberia hii leo ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya mwisho kwa nchi tatu zilizoathiriwa zaidi na mlipuko wa ugonjwa huo. Taarifa kamili na Amina Hassan.

(Taarifa ya Amina)

Katika ziara yake hiyo kwa nchi hizo, Banbury anatarajiwa kutathimini hatua za kutokomeza Ebola na maeneo ambayo Umoja wa Mataifa unaweza kusaidia zaidi. Mkuu huyo wa UNMEER anatarajiwa kukutana na Rais wa Liberia Ellen Johnson-Sirleaf pamoja na wafanyakazi wa UNMEER na ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNMIL.

Wakati Banbury akianza ziara hiyo, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linafanya kampeni ya nyumba kwa nyumba kutoa elimu kuhusu Ebola na utapiamlo mjini Monrovia mji mkuu wa Liberia kama anavyoelezea mmoja wa wanufaika Bi Josephine ambaye mwanaye anahudumiwa katika kituo cha lishe cha UNICEF.

(SAUTI JOSEPHINE)

‘’Tangu aanze kwenda katika kituo cha lishe, anaendelea vyema. Anacheza peke yake na kukaa peke yake sasa’’

Mkuu huyo wa UNMEER pia atazitembelea Sierra Leon na Guinea.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud