Haki ya watu wenye ulemavu wa ngozi albino

26 Disemba 2014

Tamko Umoja wa Mataifa  la haki za binadamu ni nguzo muhimu katika kulinda, na kutetea haki za makundi yote katika jamii kwa kuzingatia heshima na utu wa binadamu yeyote popote alipo.Tamko hilo la mwaka 1948 limetiliwa saini na nchi mbalimabli duniani wakiahidi kulinda haki za watu wao katika Nyanja mbalimbali. Miongoni mwa makundi yanayopaswa kulindwa ni watu wenye ulemavu ambao mara kadhaa hawatendewi haki kutokana na hali zao. Watu wenye ulemavu wa ngozi yaani albino ni sehemu ya kundi hilo. Nchini Tanzania kundi hili limeripotiwa kukumbana na madhila kadhaa ikiwamo kuuliwa au kukuatwa viungo kwa kile kinachodaiwa kuwa ni Imani ya kishirikina ya kwamba viungo vya albio vyaweza kutajirisha.

Tuma Dandi wa radio washirika radio Malimani ya Dar es salam Tanzania ametafiti masahibu wanayokumbana nayo albino nchini humo.

(Studio pkg)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud