Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bodaboda, muziki vyatumika kusambaza elimu ya Ebola

Waendesha pikipiki katika harakati za kuelimisha watu kuhusu Ebola.(Picha ya WHO/videocapture)

Bodaboda, muziki vyatumika kusambaza elimu ya Ebola

Huko Afrika Magharibi, mbinu mbalimbali zinatumiwa katika kuhakikisha elimu ya mapambano dhidi ya Ebola inawafikia walengwa. Miongoni mwa mbinu hizo yakinifu ni kwa kupitia wanamuziki ambao wanafikisha ujumbe kirahisi kwa jamii kupitia tasnia ya burudani.

Mbali na mbinu hiyo Umoja wa Mataifa kupitia shirika la afya ulimwenguni WHO, kwa kushirikiana na serikali ya Sierra Leon wanatumia pikipiki maarufu kama bodaboda katika kufikisha elimu kwa umma. Ungana na Joseph Msami katika Makala inayofafanua vyema makabiliano haya dhidi ya homa kali ya Ebola.