Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban alaani kufukuzwa kwa maafisa wa UM Sudan

Ban alaani kufukuzwa kwa maafisa wa UM Sudan

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amelaani hatua ya Serikali ya Sudan ya kuwafukuza  maafisa wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa nchini humo. Taarifa zaidi na Abdulahi Boru.

(TAARIFA YA ABDILAHI)

Bwana Ban amelaani hatua hiyo iliyoshuhudia kufukuzwa nchini humo kwa Mratibu Mkaazi wa Umoja UM, mratibu wa misaada ya kibinadamu, pamoja na Mkurugenzi wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa  maendeleo UNDP nchini Sudan.

Katika taarifa, Katibu Mkuu amesema kitendo cha  kuwafukuza  wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa waliotumwa nchini Sudan kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa hakikubaliki.

Aidha, Katibu Mkuu ametoa wito kwa Serikali ya Sudan kubadili uwamuzi wake mara moja na kusihi Sudan kurejesha ushirikiano wa kikamilifu na Umoja wa Mataifa.