Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kay alaani shambulizi katikakambi ya AMISOM huko Somalia

Askari wa kikosi cha Afrika kinacholinda amani nchini Somalia, wakilinda daraja la mto Juba lililotwaliwa kutoka kwa Al shabaab. (Picha:AU/UN/IST/Mahamud Hassan)

Kay alaani shambulizi katikakambi ya AMISOM huko Somalia

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini  Somalia, Nicholas Kay, amelaani shambulizi dhidi ya  kambi ya ujumbe wa Muungano wa Afrika nchini Somalia, AMISOM, ilioko katika uwanja wa Kimataifa wa Mogadishu hapo jana.

Katika taarifa yake , Bw Kay amelaani shambulizi hilo la Makao Makuu ya AMISOM mjini Mogadishu huku akipongeza juhudi za haraka za AMISOM katika kukabiliana na shambulizi hilo.

Halikadhalika, Bw Kay ametoa salamu za rambirambi kwa familia na marafiki wa askari wa AMISOM na raia ambao wamepoteza maisha yao akiwatakia wale waliojeruhiwa kupata ahueni ya haraka.

Aidha, Kay amesema azimio la Umoja wa Mataifa ni kuwasaidia watu wa Somalia katika kujenga taifa imara lenye amani.

Aleem Siddique ni msemaji wa UNSOM

(Sauti ya Aleem)