Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afrika ichukue hatua kukabiliana na madhara ya mabadiliko ya tabia nchi : Mtaalam

Mabadiliko ya tabianchi yanasababisha kuyeyuka kwa mabarafu kwenye ncha za dunia na kusababisha visiwa kuzama. (Picha:UNEP)

Afrika ichukue hatua kukabiliana na madhara ya mabadiliko ya tabia nchi : Mtaalam

Katika muktadha huo huo wa majanga yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi, imeelezwa kuwa licha ya bara la Afrika kukabiliwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa rasilimali fedha na teknolojia  katika kupambana na madhara ya mabadiliko ya tabia nchi bara hilo lazima lijitutumue ili kupunguza madhara hayo, amesema Mkurugenzi wa Mazingira ofisi ya makamu wa Rais wa Tanzania Dk Julius Ningu.

Akihojiwa na idhaa hii kuhusu hatma ya athari za mabadiliko ya tabia nchi kwa Afrika Dkt Ningu anasema nini kifanyike kwanza ili kuchukua hatua japo kwa kuchechemea.

(SAUTI NINGU)

Kadhalika amezungumzia nafasi ya wahisani katika kusaidia bara la Afrika kupambana na madhara ya mabadiliko ya tabia nchi.

(SAUTI NINGU)