Mwongo Moja tanguTsunami tumejifunza kukabiliana na majanga ya asili. UM

26 Disemba 2014

Leo ni miaka Kumi tangu mataifa katika ukanda wa Kusini na Kusini Mashariki mwa Asia, kukumbwa na Tsunami ya Bara Hindi ambapo zaidi ya watu laki mbili  walipoteza maisha yao. Taarifa zaidi na Amina Hassan.

(TAARIFA YA AMINA)

Janga hilo lilosikika katika karibu pembe zote za dunia, lilidhirisha vyema jinsi dunia ilivyo dhaifu katika kukabiliana na majanga ya kiasili kando na kuweka bayana umuhimu wa kukabiliana na majanga haya ana kwa ana kwa kuimarisha maandaalizi  mema na yakijasiri.

Kwa muktadha huo, janga hili liliibua juhudi mpya za kimataifa za kupunguza hatari, ya maisha na uharibifu wa kiuchumi utokanao na majanga ya kiasili.

Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kupunguza maafa hatari, UNISDR, Margareta Wahlström amesema Miaka kumi baada ya Tsunami ya Bahari ya Hindi, dunia imechukua hatua muhimu kufanya dunia kuwa mahali salama dhidi ya majanga.

Halikadhalika, Bi Wahlström amesema kwa sasa kuna ufanisi zaidi wa mifumo ya onyo la mapema na utaratibu bora wa uokoaji .

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter