Baada ya Miaka Kumi Banda Aceh imechukua hatua: UM

26 Disemba 2014

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto, UNICEF, limepongeza watu wa Aceh, Magharibi mwa Indonesia kwa ujasiri na mafanikio yao katika kupambana na uharibifu uliotokana na Tsunami.

Mwakilishi wa UNICEF nchini Indonesia, Gunilla Olsson amesema juhudi kubwa ya watu wa jimbo la Aceh wakisaidiwa na jumuiya ya kimataifa katika kujenga upya maisha yao kabla ya kuharibiwa na mawimbi imefanikiwa.

Bw Olsson amesema kuwa juhudi hizo zilizohimiza kanuni ya ujenzi bora zimeleta ufanisi kwa watoto kuwa na afya na kuendeleza vipaji vyao.

Tomi Soetjipto ni Msemaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP.

(SAUTI TOMI)

"Kuna mambo mawili ambayo Aceh walitekeleza vizuri kwanza ni uamuzi a serikali ya Indonesia kuanzisha shirika la kusimiamia urekebishaji baada ya Tsunami ambalo linaongozwa na mtu aliye na uzoefu na ambaye anaripoti moja kwa moja kwa rais na hivyo kuwezesha juhudi za haraka, la pili ni kwamba wakati hatua ya dharura ilipofika serikali ilikuwa tayari imeweka msingi thabiti wa ukarabati kwa hivyo iliwezesha kutoka katika hatua ya dharura hadi ile ya ukarabati."

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter