Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ustawi wa wanawake Afrika Mashariki

Mwanamke akinywesha miche katika eneo la Ziwa Tana, eneo la Ahara, Ethiopia. Picha: IFAD / Petterik Wiggers(UN News Centre)

Ustawi wa wanawake Afrika Mashariki

Jarida letu maalum leo linaangazia juhudi za wanawake katika kujikwamua kiuchumi hususani katika jamii ambazo zimekumbana na mizozo.Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wanawake UNWOMEN kupitia mkuu wake Pumzile Mlambo Ngucka limetaka mwaka 2015 dunia iunge mkono juhudi za ustawi wa kundi hilo ambapo Bi Ngucka amekaririwa akisema kuwa mwaka ujao uwe wa kuhakikisha usawa wa kijinsia unakuwwepo katika nyanja zote ikwamo uchumi.Kwa mantiki hiyo wanawake wenyewe wanapaswa kuwa mstari wa mbele ili kukuza hamasa miongoni mwa jamii na kisha kuungwa mkono na makundi mengine wakiwamo wanaume.   Katika kumulika juhudi za wanawake kujikomboa kiuchumi tunaanzia huko Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo DRC ambapo tunaaungana na Langi Asumani kutoka radio washirika Radio Umoja iliyoko jimbo la Kivu Kusini.

(Studio pkg)