Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNSMIL yalaani mauaji ya Daktari wa Coptic Kutoka Misri na kutoa wito kurejeshwa Bintiye salama.

Nembo ya UNSMIL

UNSMIL yalaani mauaji ya Daktari wa Coptic Kutoka Misri na kutoa wito kurejeshwa Bintiye salama.

UNSMIL imesema katika taarifa yake kuwa kitendo cha mauwaji maovu yanayokisiwa kutekelezwa kwa misingi ya kidini  na watu waliojihami wasiojulikana hakikubaliki kabisa na watu wa Libya na kwamba vitendo kama hivyo ni vigeni na haviambatani na mila za jamii ya Libya ya kuvumilia watu wa jamii ya dini walioawachahe na kuwakubali wengine kwa ukarimu.

Kwa hiyo, UNSMIL imetoa wito kwa mamlaka na watendaji walio na ushawishi mkubwa, raia na viongozi wa kidini, kuingilia kati haraka ili kuhakikisha kwamba msichana aliyetekwa ni huru bila kudhuriwa  na kwamba mauaji hayo yatachunguzwa vizuri na wahusika kufikishwa mahakamani.