Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashirika ya Misaada yapigia Chepuo masomo Sudan Kusini

Huyu ni msichana Natabo Gabriel,huko Sudan Kusini akiwa na cheti baada ya kuhitimu jimbo la Equitoria(Picha© UNICEF South Sudan/2014/Ligoo)

Mashirika ya Misaada yapigia Chepuo masomo Sudan Kusini

Kaimu mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS, Toby Lanzer ameonya kuwa mustakbali wa nchi hiyo uko mashakani kama sekta ya elimu itaendelea kuathiriwa na mgogoro unaoendelea. Taarifa kamili na Amina Hassan.

(Taarifa ya Amina)

Lanzer ameomba pande zote katika mgogoro wa nchi hiyo kufanya juhudi kupeleka watoto shuleni mwaka wa 2015 na kuheshimu wafanyakazi wa kutoa misaada.

Akitolea mfano wa vitu ambavyo vinahitajika wanafunzi kurudi shuleni, Bw Lanzer amesema japo kuwarejesha wanafunzi shule inahitaji mambo mengi, lakini wakati mwingine ni kuwepo kwa vitu vya kimsingi kama ubao na chaki au kurekebishwa kwa paa la darasa liliobomoka linatosha.

Kuhusu misaada ya Mashirika ya Umoja wa Mataifa katika kuboresha hali ya elimu nchini, Bw Lanzer amesema

(SAUTI LANZER 10’’)

Najua kwamba mashirika muhimu kama vile UNICEF na UNESCO wanafanya bidii kuhusiana na suala hili lakini pia kuhusu suala nzima la kujua kusoma na kuandika”

Hata hivyo Lanzer ameonya kuhusu hatima ya nchi hiyo bila uwekejazi katika elimu.

(SAUTI LANZER )

"Ukweli unaosikitisha ni kuwa Sudan Kusini haitaweza kwenda mbali katika siku zijazo kama asilimia 80 ya watu hawawezi kusoma wala kuandika. Hebu tuwe wakweli kuhusiana na hili."