Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

JICA yaipiga jeki UNRWA

Picha:UNRWA

JICA yaipiga jeki UNRWA

Shirika la Maendeleo la Japan JICA limetoa msaada wa madawa kwa ajili ya kutakatisha maji kwa wananchi wa Palestina.

 Msaada huo uliopokelewa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi wa Palestina UNRWA  utawanufaisha wananchi walioko katika Ukanda wa Gaza ambao unakabiliwa na changamoto mbalimbali.

 Akizungumza baada ya kupokea msaada huo Mkurugenzi wa UNRWA katika Ukanda wa Gaza Robert Turner alilishukuru shirika hilo la Japan ambalo alisema kuwa daima limekuwa mstari wa mbele kuwasaidia wananchi wa Palestina.

 Eneo hilo la Gaza ni maskani ya raia wengi na karibu wakazi 19,000 waliokosa makazi wanategemea msaada kutoka UNRWA.