Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

“2015 uwe mwaka wa mwanga na nuru” UNESCO

Dira ya dunia@UNESCO/NASA

“2015 uwe mwaka wa mwanga na nuru” UNESCO

Shirika la Sayansi,Elimu na Utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO limesema kuwa mwaka 2015 unapaswa kuwa mwaka wa matumaini na tena ni mwaka wenye kuleta nuru pale kwenye giza.

Likichangiza harakati za mwanasayansi wa zamani Isaac Newton aliyewasha mshumaa na kutafsiri rangi zilizojitokeza, UNESCO imesema Umoja wa Mataifa umeutangaza mwaka 2015 kuwa ni mwaka wa nuru na kwamba nuru hiyo inakwenda sambamba na utambuzi wa teknolojia, amani endelevu na ukuzaji wa elimu

 Ili kukamilisha hatua hiyo, UNESCO imepanga kuwaleta pamoja watu wa matabaka ya aina mbalimbali ikiwamo wanasayansi, wataalamu wengine, mashirika ya kiraia na taasisi za kiraia kwa ajili ya kujadiliana na kuangazia mwaka huo.

Akizungumza na idhaa hii Katibu mtendaji wa tume ya taifa ya shirika la Umoja wa Mataifa la elimu sayansi na utamaduni UNECSO nchini Tanzania Dkt. Moshi Kiminzi amezungumzia umuhimu wa tamako hili la UNESCO.

(SAUTI KIMINZI)