Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN yapongeza Liberia kwa kufanya uchaguzi kwa amani

Uchaguzi nchini Liberia(Picha ya UM/Unifeed vido capture)

UN yapongeza Liberia kwa kufanya uchaguzi kwa amani

Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa ambaye anaratibu operesheni za misaada nchini Liberia Karin Landgren amesema kuwa hatua iliyochukuliwa na wananchi wa Liberia waliojitokeza kwa wingi kwenye upigaji kura ni hatua ya kuridhishwa na pia inaonyesha jinsi wananchi hao walivyoamua kulijenga taifa lao.

Wananchi hao walijitokeza kwa wingi katika uchaguzi wa maseneta uliofanyika Disemba 20 nchini kote. Hadi sasa zoezi la ujumulishaji matokeo bado linaendelea.

Mjumbe huyo amewapongeza wananchi hao akisema kuwa wamechukua jukumu la kuijenga nchi yao kwa njia ya kidemokrasia na utulivu wa amani.