Ban apongeza Tunisia kwa kufanikisha marudio ya uchaguzi wa Rais

23 Disemba 2014

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesema hatua kubwa imepigwa nchini Tunisia kufuatia marudio ya uchaguzi wa Rais jumapili nchini humo.

Awamu ya kwanza ya uchaguzi ilifanyika mnamo Novemba 23 ambapo hakuna mgombea aliyeshinda kwa idadi kubwa ya kura. Mgombea mkongwe Beji Caid Essebsi ameshinda awamu ya pili ya uchaguzi

Huu ni uchaguzi wa kwanza nchini Tunisia tangu mapinduzi ya mwaka 2011 yalyochochewa na kijana muuzaji wa bidhaa rejareja aliyejiteketeza kwa moto baada ya askari kumnyang’anya mkokoteni wake.

Stephane Dujarric ni msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa

"Katibu Mkuu anawapongeza watu wa Tunisia kwa kuendesha kwa mafanikio marudio ya uchaguzi wa kidemokrasia kwa ajiliya rais mnamo Desemba 21. Pia anampongeza Bwana Beji Caid Essebsi kwa kuchaguliwa kwake. Katibu Mkuu ameelezea matumaini yake kuwa watu wa Tunisia pamoja na mamlaka mpya teule itaendeleza ujumuishwaji ambao umeongoza kipindi cha mpito hadi sasa."

Katibu Mkuu amesisitiza utayari wa Umoja wa Mataifa katika kuendelea mamlaka ya Tunisia inapokabiliana na changamoto ambazo nchi inakumbana nazo ili kufanikisha mchakato wa uimarishaji wa kidemokrasia na maendeelo ya kiuchumi.

Bwana Ban pia amepongeza mamalaka ya uchaguzi nchini humo kwa kuendelea na juhudi zao katika kukamilisha mchakato

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud